The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Sabaya Yakwama Kortini

0

Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita imeahirishwa baada ya shahidi wa Jamhuri kudai bado anaumwa.

Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ramadhan Juma alitegemea kutoa ushahidi wake leo Ijumaa Oktoba 22, 2021, lakini Wakili Mwandamizi wa Serikali, Felix Kwetukia aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iahirishe kesi hadi Oktoba 27, 2021 kwa kuwa shahidi huyo afya yake bado haijaimarika.

Leave A Reply