The House of Favourite Newspapers

Kesi Ya Waandishi Waliorusha ‘Drone’ Bungeni Yaanza Kunguruma

0

KESI inayowakabili waandishi wawili wa habari wa nchini Myanmar, wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kurusha kifaa maalum kinachotumika kupiga picha kutoka angani (drone) katika jengo la bunge la nchi hiyo, imeanza kusikilizwa na mahakama kuu ya nchi hiyo huku waandishi hao wakiwa kwenye hatari ya kufungwa jela miaka miwili hadi mitatu kwa kosa hilo.

 

Waandishi hao wenye uraia wa Malaysia na Singapore, wanaofanya kazi kwenye Shirika la Habari la TRT la Uturuki, walikamatwa hivi karibuni baada ya kukiuka sheria za nchi hiyo, kwa kurusha kifaa hicho bila idhini ya jeshi la polisi, jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheria za nchi hiyo.

 

Msuguano mkubwa umetanda kati ya nchi za Mynamar na Uturuki, kufuatia mauaji makubwa ya Rohingya, jambo lililosababisha nchi hizo kufanyiana visa vya hapa na pale, kila moja ikitetea maslahi yake, Mynamar ikiwaua watu wanaodaiwa kuwa waasi, wanaojificha Rohingya huku serikali ya Uturuki inayoongozwa na Recep Tayyip Erdogan, ikisema watu hao si waasi bali Waislamu wenye msimamo mkali.

NAYPYIDAW, MYANMAR

Leave A Reply