The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kesi Wanaodaiwa Kuchana Noti 460,000 za BOT Yaahirishwa

0

KESI inayowakabili watu 13 wakiwemo watumishi wanane wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na wenzao watano imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika. 

 

Watumishi hao wanakabiliwa na mashtaka sita likiwemo la kuharibu noti 460,000 za TSH 10, 000 na kuisabaishia benki hiyo hasara ya Tsh bilioni 4.6.

 

Watumishi hao wa BOT ni Mariagoretha Kuzugala, Henry Mbowe, Asha Sekiboko, Cecilia Mpande, Agripina Komba, Zubeda Mjewa, Khadija Kassunsumo na Mwanakheir Omary. 

 

Washitakiwa wengine ni Alistides Genand, Shukuru Mchegage, Musa Chengula, Zaituni Chihipo na Respicius Ishengoma.

 

Wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu, amedai, kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamlika. 

 

Kutokana na hilo, ameiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili kutaja shauri hilo, hivyo hakimu ameahirisha shauri hilo hadi Januari 11, mwaka 2021.

 

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kwamba kati ya Januari mwaka 2017 hadi Septemba 30, mwaka 2019, watumishi hao wa BOT kwa kuvunja majukumu yao ya kazi waliwezesha utendekaji wa kosa la kuongoza genge la uhalifu bila ya kuwa na kibali na kutokuwa wazalendo, waliharibu noti kwa kukata noti 460,000 za 10,000 sawa na Sh bilioni 4.6.

 

Leave A Reply