The House of Favourite Newspapers

KESI YA WEMA PICHA ZA UTUPU, UPELELEZI WAKAMILIKA

UPELELEZI wa kesi ya kuchapisha video ya ngono kupitia ukurasa wa Instagram inayomkabili Msanii wa Filamu, Wema Sepetu, umekamilika na itaanza kusikilizwa Februari 21, mwaka huu baada ya kusomewa maelezo ya awali.

 

Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Glory Mwendi mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde. Wakili Glory ameeleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na anaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

 

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi February 21, 2019. Katika kesi hiyo namba 322 ya mwaka 2018, Wema anadaiwa Oktoba 15 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar alichapisha video za ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati akijua ni kinyume na sheria.

Comments are closed.