The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Wema Sepetu Kusikilizwa Januari 2019

Miss Tanzania 2016, Wema Sepetu

Kesi ya kusambaza picha za utupu inayomkabili Miss Tanzania 2016, Wema Sepetu imetajwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kuahirishwa hadi Januari 28, 2019.

 

Upande wa Jamhuri  ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Mosia Kaima,umedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wakati kesi hiyo ilipokuja mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde kwa ajili ya kutajwa.

 

Kaima aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kuitaja ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

 

Hakimu  baada ya kusikiliza maelezo hayo aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 28 mwakani 2o19, itakapotajwa tena.

 

Katika kesi hiyo, Wema anadaiwa kuwa Oktoba 15, mwaka huu katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Comments are closed.