The House of Favourite Newspapers

Kesi Zuio la Uchaguzi TFF Yatupiliwa Mbali

0

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, jana Ijumaa ilitupilia mbali maombi ya kuzuia Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yaliyowasilishwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais, Ally Saleh.

 

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa kutupilia mbali kesi ya kuzuia uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu jijini Tanga.

 

Ally Saleh alifungua kesi hiyo dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Wajumbe wa Bodi.Ikumbukwe kuwa, mara baada ya mchakato wa usaili kumalizika na rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia kubaki peke yake kwenye kuwania nafasi hiyo, ndipo ikafunguliwa kesi hiyo ya kuzuiwa kwa uchaguzi.

 

Mbali ya nafasi ya urais, kuna nafasi sita za kamati ya utendaji zinawaniwa.

Leave A Reply