The House of Favourite Newspapers

KESSY: 2020 Upinzani Mtapata Aibu Kubwa, Kura Zote CCM – Video

 

Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kessy akichangia hoja bungeni leo kuhusu Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano amemuomba Waziri Prof. Makame Mbarawa kusimamia ujenzi wa barabara ya Kirando Kazovu ambayo imechukua takribani mwaka mzima hali iliyosababisha vifo vya watu watatu.

 

Kessy amesema mpaka sasa wanafunzi wanashindwa kwenda shule kutokana na ubovu wa barabara hiyo hivyo Serikali ifanye jitihada kuitengeneza ili kuoberesha miundombinu hiyo kwa wakazi wa eneo hilo..

 

Aidha, Kessy ameipongeza Serikali ya Rais Magufuli kupitia Wizara ya Ujenzi kwa kufanikisha ujenzi wa barabara na miundombinu mingine katika wilaya yake ya Nkasi huku akisema wapiga kura wa jimboni kwake wamesema waziwazi kwamba hawahitaji upinzania tena, wameahidi kuipa kura CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.

MSIKIE KESSY AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.