The House of Favourite Newspapers

Kessy anaivaa Yanga kwa staili mpya ya nywele

0

BEKI wa kulia wa Simba, Hassan Kessy, tayari amejiandaa kuikabili Yanga leo huku akiwa na staili mpya ya mtindo wa nywele ambayo ni maalum kwa mechi ya leo tu.

Simba na Yanga zitapambana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika muendelezo wa Ligi Kuu Bara. Timu zote zilikuwa kambini visiwani Zanzibar ambapo Yanga ilikuwa Pemba na Simba Unguja.

Kessy amenyoa mtindo unaofanana na kiduku ambao huondoa nywele za pembeni ya kichwa na kubakiza za katikati kuanzia mbele ya kichwa hadi nyuma.

Katika mtindo huo mpya, Kessy amenyoa nywele zote na kuzibakisha kidogo katikati ya kichwa.

Mtindo huu unamfanya Kessy aonekane tofauti kidogo awapo uwanjani na alipoulizwa sababu ya kunyoa hivyo alisema: “Kinyozi wangu ndiye aliyeniambia ninyoe hivi ili nionekane tofauti katika mchezo huu.”

Leave A Reply