The House of Favourite Newspapers

KEVIN DURANT HATARINI KUONDOKA WARRIORS

Kevin Durant

BAADA ya misimu miwili ya mafanikio akiwa na mabingwa, Golden State Warriors, staa wa timu hiyo, Kevin Durant ameanza kutajwa kuwa anaweza kuondoka mapema tofauti na inavyotegemewa. Durant amekuwa na mchango CALIFORNIA, Marekani

mkubwa kikosini hapo lakini inavyoonekana anaweza kuondoka msimu ujao ambapo atakuwa mchezaji huru na taarifa za ndani ya timu hiyo zinaeleza kuwa mipango hiyo ipo japokuwa mwenyewe hajajitokeza kuthibitisha.

 

Haijajulikana akiamua kuondoka ataenda wapi, japo kuna taarifa kuwa anaweza kuungana na rafiki yake wa muda mrefu, LeBron James katika timu ya Los Angeles Lakers au kurejea nyumbani kwao kujiunga na Washington D.C.

Comments are closed.