Kevin Hart Ajeruhiwa Vibaya kwa Ajali ya Gari
Ajali hiyo ilitokea katika Barabara Kuu ya Mulholland ambapo gari la Kevin, aina ya Plymouth Barracuda, lilitoka barabarani na kuingia kwenye mtaro na kuparamia ua wa magogo na hivyo sehemu ya juu ya gari kuharibika vibaya.
Wawili hao walikimbizwa hospitali, ikiwa ni baada ya Kevin kujinasua katika gari hilo na kwenda kupata matibabu katika makazi yake.
Hart alilinunua gari hilo mwezi Juni mwaka huu akijizawadia kutimiza miaka 40 ya kuzaliwa kwake.
Comments are closed.