Khadija Kopa: Aanika Hasira za Zuchu

MAMA mzazi wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Zuhura Othman Kopa ‘Zuchu’, Khadija Kopa amefichua siri kumhusu bintiye kwamba ana hasira za haraka pindi mtu anapomkera.

 

Akipiga stori mbili tatu na Risasi Vibes, Malkia huyo wa Mipasho Bongo, alisema kwamba alimlea mwanaye katika mazingira bora na ya kujituma, lakini mbali na vyote hivyo, mtoto wake amekuwa ni mtu mwenye hasira za karibu pindi inapotokea kakasirishwa.

 

“Nidhamu na upendo mnaouona leo hii kwa Zuchu, ni matokeo mazuri ya malezi yangu bora kwake, ni mtoto mzuri mwenye kujali na kumthamini kila mtu, lakini pia ni binti ambaye ana hasira sana kwa watu wasiomjua hasa inapotokea umemkera huwa hawezi kujizuia,” alisema Kopa.

STORI  | Memorise Richard, Risasi

 

Toa comment