Khalid Aucho Afungiwa Kutocheza Michezo Mitatu Na Faini Ya Sh500, 000
KIUNGO wa Yanga, Khalid Aucho leo Novemba 17, 2023 amefungiwa kutocheza michezo mitatu na faini ya Sh500, 000 (laki tano)
Kufungiwa nyota huyo ni kutokana na kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Ibrahim Ajibu wa Coastal Union Novemba 8, 2023 katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mchezo huo pia Coastal Union imetozwa Sh1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la wachezaji kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia nguo, jambo lililosababisha mchezo kuchelewa kuanza kupindi cha kwanza na baada ya mapumziko, hivyo kuharibu program za mrusha matangazo ya runinga (Azam TV) ambaye ni mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga
Aucho atakosa mechi ya Mtibwa Sugar Disemba 16, Tabora United Disemba 22 na 26 dhidi ya Kagera Sugar.