Khloe Kardashian, James Harden kila mtu kivyake

Khloe-Kardashian-1LOS ANGELES, Marekani
WADAKU wanasema Khloe Kardashian amemtema mpenzi wake ambaye ni mcheza kikapu wa Klabu ya Houston Rockets inayoshiriki NBA, James Harden baada ya kuwa naye kwenye uhusiano kwa miezi kadhaa.

Khloe na James kwa pamoja walikuwa msaada mkubwa kwa mume wa mrembo huyo, Lamar Odom alipolazwa baada ya kupoteza fahamu kwa madai ya kutumia dawa za kulevya kuzidi kiwango huko Nevada Oktoba mwaka jana.

james-harden-houston-rockets-nbaChanzo cha ndani cha wapendanao hao kimesema kuwa; “Alimtema wiki kadhaa zilizopita.”
Lakini Khloe amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kama Instagram kutoa mistari mbalimbali ambayo wachambuzi wa burudani wanadai kuwa ni ujumbe kwenda kwa James.

“Kila kitu kinatokea kwa sababu. Unapoteza ili upate. Maumivu au machungu yanakujengea nguvu, moyo, tabia na amani,” aliandika Khloe.

Kisheria Khloe ni mke halali wa Lamar Odom inadaiwa kuwa hakuna chochote kinachoendelea cha kimapenzi kati yao kwa sasa zaidi ya kuwa marafiki tu.

Loading...

Toa comment