KIAMA CHA WAKINA GIGY MONEY, SANCHI, AMBER LULU KIMEFIKA

Lulu Euggen ‘Amber Lulu.

“HATUWEZI kuwa na wanamuziki wanaotegemea kiki, niombe kwa wasanii wote wanaotegemea muziki wao kwa kiki waache mara moja.”

 

Ni maneno ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alipokuwa akizungumzia video ya msanii na muuza nyago kwenye video za Kibongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ ambayo ilitambaa mitandaoni ikionekana wazi kukosa maadili.

Yes! Kiki limekuwa jambo la kawaida sana kwa wasanii wa filamu na muziki. Wengi wanaamini bila kufanya hivyo kazi zao haziwezi kupokelewa kwa kishindo na mashabiki wao! Ingawa ni ukweli usiofichika kwamba kwa ulimwengu wa sasa kiki ni sehemu ya kumuinua msanii, lakini kiki zinazofanyika kwa soko la muziki wa Bongo Fleva ni tofauti. Wasanii wapo tayari kufanya tukio la kudhalilika hadharani ili lengo lao litimie, huu ni upuuzi uliopitiliza!

 

BASATA Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) mara kwa mara limekuwa likiwaita wasanii hawa na kukaa nao, lakini kesho na keshokutwa linajirudia hadi najiuliza wanawaita kufanyaje sasa? Siwezi kuwasemea sana, lakini mara nyingi huchukua hatua pale tukio linapokuwa limeshatokea na kuchafua hali ya hewa na wakati mwingine husema kuwa mhusika aliyefanya hivyo hawamtambui kwa sababu hajasajiliwa kwao, seriously?

Jane Rimoy ‘Sanchi’

SANCHI

Mwaka jana mwanamitindo Jane Rimoy ‘Sanchi’ alisumbua kwa kutupia picha zake mitandaoni zilizoonekana kukosa maadili na Basata wakaahidi kulifungia kazi, hadi leo sitaki kulizungumzia lilipoishia maana ninachoendelea kukiona mtandaoni kwa huyu dada temea mate chini!

 

AMBER LULU

Nimemsikia vizuri Waziri Shonza akiapa kudili na hawa wapenda kiki kwa maana ya wasanii wanaoji-dhalilisha mtandaoni kwa lengo ya kusogeza kazi zao, safi sana! Waziri Shonza alikuwa akizungumza na mmoja wa viongozi wa Basata na kuulizia kama wameiona video ya Amber Lulu na wameshaifanyia kazi au la! Jibu lililotoka ni kwamba wameiona na wameshamuandikia barua ya kumuita, jambo alilolipokea vizuri na kusema kama wangekuwa hawajafanya hivyo angemuita haraka na kuchukua hatua yeye mwenyewe.

 

SISTER FEY

Ukiachana na Amber Lulu, Sister Fey ambaye ni msanii wa Bongo Fleva naye amekuwa akifanya kiki mtandaoni hadi anapitiliza. Mwaka jana, Waziri Shonza aliiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kumfuatilia msanii huyo juu ya matumizi yake ya mitandao na hatimaye alikamatwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar. Waziri Shonza alisema alitegemea huenda Fey angebadilika mwenendo wa tabia yake hiyo, baada ya kuitwa na Basata kwa mara ya kwanza badala yake alizidisha.

 

GIGY MONEY

Huwezi kuwataja wanaofanya kiki kwa kujiachia nusu utupu mitandaoni jina la Gigy Money likakosekana! Alivyojiingiza katika muziki wengi waliona huenda akabadilika, lakini ndiyo kwanza amekuwa akifanya yaleyale kama ya Amber Lulu. Mwaka jana pia, Waziri Shonza alidili naye ambapo alimtaka kufika ofisini kwake kwa kuwa alitumiwa ujumbe wa wito hakufika.

 

AMBER RUTTY

Achana na anavyojifananisha na Amber Lulu, amejipatia jina baada ya video zake chafu kusambaa akionekana na mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Said Mtopali. Amber Rutty amekuwa akichafua mitandaoni mara kwa mara na video chafu huku akiachia nyimbo zake. Tayari Basata wamejitoa kwa kusema kuwa hawamtambui kama msanii kwa sababu hajasajiliwa kama msanii au kiku

 


Loading...

Toa comment