The House of Favourite Newspapers

Kiba anaswa akimvutisha Ne-yo mambo!

0

Aache mambo yake! Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amenaswa akimvutisha ‘mambo’ mwanamuziki mwenye ‘taito’ kubwa duniani kutoka Marekani, Shaffer Chimere Smith ‘Ne-Yo’.

Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Viwanja vya Kriketi vya Lugogo jijini Kampala nchini Uganda walipokuwa wakifanya makamuzi kwenye shoo iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia Uganda (UBL) ya nchini humo.

Kiba ni msanii pekee kutoka Tanzania aliyebahatika kupewa shavu la kufanya shoo hiyo kwenye jukwaa moja na Ne-Yo.

Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, kufuatia ukaribu wao, Kiba alimshawishi rafiki yake huyo na kumvutisha mambo a.k.a shisha.

Chanzo hicho kilivujisha ubuyu kwamba, Kiba alipata shavu hilo la kufanya makamuzi baada ya kupendekezwa na Ne-Yo, siku chache baada ya kuonana jijini Nairobi, Kenya walipokutana kwenye Tamasha la Coke Studio, hivyo ukaribu wao na picha walizokuwa wakipiga kwa pamoja ziliwafanya baadhi ya mashabiki wa Uganda kumtaka ajumuike naye kwenye shoo hiyo.

Ilisemekana kwamba, kwa namna walivyokuwa wakishirikiana, mashabiki wa Uganda walijikuta wakitamani kuwaona kwenye shoo ya pamoja ambayo ilisababisha gumzo kubwa kiasi cha wengi kuamini uwepo wao umesababisha mapinduzi ya burudani nchini humo.

“Matukio yalikuwa mengi kwani Kiba alionesha hali ya kukubalika sana kwa Ne-Yo, maana muda mwingi walikuwa wote wakifurahi hadi kufikia hatua ya kuvutishana shisha, jambo ambalo mashabiki na watu waliokuwa wakiwashuhudia walimshangaa King Kiba kwa kufanikiwa kumvutisha jamaa huyo kilevi hicho,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:

“Pamoja na kufanya shoo ya pamoja, kesho yake walizama studio na kufanya ngoma ambayo ni ya King Kiba, naamini itakuwa nzuri na kali kwani ushirikiano waliouonesha ulikuwa mkubwa,” kilisema chanzo chetu kutoka Uganda.

Leave A Reply