KIBA KAMA MFALME OMAN!

DAR ES SALAAM: Hii ni zaidi ya historia! Mkali wa Bongo Fleva, Ally Salehe Kiba ‘AliKiba’ amejitengen­ezea heshima baab’kubwa baada ya kupata mapokezi ya nguvu, nchini Oman alipokwenda kufanya shoo.

Mkali huyo aliwasili nchini humo katikati ya wiki iliyopita ambapo ali­pumzika kwenye hoteli ya nyota tano kabla ya kukinukisha katika ukumbi wa hoteli hiyo aliyofikia ijulikanayo kwa jina la InterContinental, Muscat wikiendi iliyopita.

 

 

MAPOKEZI YAKE

Mtanzania aishiye Muscat, Abdulh­man Jumaa ambaye alikuwa mmoja wa watu walioshuhudia mapokezi ya Kiba, amezungumza na Ijumaa Wikienda moja kwa moja kwa njia ya simu ambapo alisema jamaa amepata mapokezi ambayo hajawahi kuyaona kwa msanii yeyote kutoka Bongo.

 

“Nipo Oman kwa zaidi ya miaka nane sasa, sijawahi kuona mapokezi ya msanii kutoka Bongo ya namna hii, Kiba amevunja rekodi. Yaani Watan­zania na hata wasio Watanzania, wamempa uspesho fulani mwanzo mpaka mwisho utafikiri mfalme vile jinsi walivyomheshimu.

 

 

DIAMOND TUPA KULE

“Nimeona Diamond alikuja mwaka juzi kama sikosei akafanya uwanjani lakini mapokezi yake yalikuwa ya kawaida sana si kama haya ya Kiba, nafikiri huku wanamuelewa zaidi Kiba kuliko Mondi,” alisema Jumaa.

 

SHAMRASHAMRA KAMA ZOTE

Alisema, kuanzia wanatoka Airport hadi wanafika kwenye hoteli waliyoan­daliwa kwa ajili ya kupumzika, Kiba alipewa msafara mkubwa uliokuwa na magari ya kifahari yasiyopungua 10.

“Yaani ilikuwa balaa kuanzia Air­port, watu walimzonga kwelikweli wakitaka kupiga naye picha. Alijitahidi kupiga na baadhi ya mashabiki wake kabla hajaingia kwenye msafara wake uliokuwa na magari ya kifahari tupu,” alisema.

 

 

VIDEO YAKE USIPIME

Kuonesha msisitizo, Jumaa alimtumia mwanahabari wetu video ambayo inamuonesha Kiba akiwa kwenye gari la kifahari la kufunuka juu huku akifuatiwa na magari mengine ya kifahari kuelekea hotelini.

 

SHOO BAAB’KUBWA

Ijumaa Wikienda kupitia vyanzo mbalimbali, lilifani­kiwa kupata picha mbalimbali za shoo hiyo aliyoifanya Kiba kwenye Hoteli ya InterContinental am­bapo ilikuwa ‘imefunga watu hatari’.

Kwenye shoo hiyo, Kiba alipafomu nyimbo zake zote ikiwemo Aje hadi hii ya sasa ambayo ni kama ya taifa, Kadogo.

Alipoimba wimbo huo, licha ya kuwa ni mpya Bongo, mashabiki walioneka­na kuufurahia na kuimba naye utafikiri una mwaka kumbe ndio kwanza una miezi miwili tu na ushee.

 

Shuhuda mwingine aliyeishuhudia shoo hiyo ambaye ni Mtanzania, aliliambia gazeti hili kuwa, Kiba amefanya shoo kali ya kufungulia mwaka na kuandika rekodi ya aina yake.

“Hii kwa hapa Mascat ameacha gumzo. Kila mtu anamzungumzia Kiba, kuna ambao walikuwa ha­wafahamu ndio wamemuona kwa mara ya kwanza, yaani wanatamani kumuona tena na tena,” alisema Aisha Khamis.

 

MENEJA AFUNGUKA

Ijumaa Wikienda lilizun­gumza na mmoja wa mameneja wa msanii huyo aitwaye Aidan Seif ambapo alipoulizwa kuhusu mafanikio ya shoo hiyo, alisema anamshukuru Mungu imefanikiwa na kwamba ni muendelezo wa Kam­puni ya Rockstar4000 kumuandalia Kiba pamoja wasanii wengine wa lebo hiyo shoo kubwa nje ya nchi.

 

Alisema mpaka sasa, wamesha­fanya shoo nyingi kubwa nje ya nchi na wanaende­lea kupokea mialiko hivyo wanam­shukuru Mungu na Watanzania kwa kuendelea kumsapoti Kiba kwani uzalendo unaanzia nyumbani.

 

“Unajua bila Watanzania, Kiba muziki wake usingependwa nje kama hivi tunavyopokea mialiko kila kukicha, tunaomba waendelee ku­tusapoti. Kiba amefanya vizuri sana Oman, watu wameruka mwanzo mwisho hivyo nina amini picha kama hii itatokea maeneo mbalim­bali,” alisema Aidan.

Stori: Erick Evarist, Dar

Loading...

Toa comment