KIBA, MCHUMBA WA MONDI WAIBUA GUMZO

 DAR ES SALAAM: Habari ‘hot’ kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo ni kuhusu msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz au Mondi’ kutangaza uhusiano mpya na mrembo kutoka Kenya, Tanasha Donna Barbieri ‘Zahara Zaire’ huku gumzo jipya likiibuka baada ya kubainika kuwa, Tanasha ni yule aliyewahi kudaiwa kutoka na mwanamuziki Ally Sahehe Kiba ‘Alikiba’ mwaka 2015.  

 

Diamond ambaye ni Mkurugenzi wa Wasafi Classic Baby (WCB) akiwa kwenye ziara ya Tamasha la Wasafi Festival mkoani Mtwara hivi karibuni alitangaza kunasa kifaa kipya kitakachoziba pengo la Zarinah Hassan ‘Zari’ na akamtaja Tanasha ambaye ni mtangazaji wa redio moja maarufu nchini Kenya.

 

Akasema kuwa, mrembo huyo ana kila sifa ya kuwa mkewe kuwashinda akina Lilian Kessy ‘Kim Nana’ na Irene Godfrey ‘Lynn’ ambao wamekuwa wakitajwa kugombania nafasi kwa rais huyo wa WCB.

 

“Tanasha ndiye mwanamke pekee aliyeonesha kujali hivyo rasmi natangaza kumuoa. Ana sifa zote za mwanamke wa kuoa, lakini unajua sisi wanaume wengi huwa tunaangalia sura, umbo na vingine vya mwilini kisha ndiyo  inafuata tabia. “Lakini nimejiridhisha kwamba mbali na umbo na mvuto wa kipekee pia ni mwanamke mwenye tabia nzuri,” alisema Diamond alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni.

TEAM KIBA ‘WAFUKUA MAKABURI’

Baada ya Diamond kujinasibu kupata mchumba mpya huku akimmwagia sifa kidekede, mashabiki wa Alikiba ‘Team Kiba’ waliibuka kutoka kusikojulikana na kuanza kuponda penzi hilo jipya mitandaoni wakisema kuwa, msanii wao ameshapita huko, Diamond anakula ‘makombo’.

 

Team Kiba hao wamekuwa wakitoa povu sambamba na kuachia picha kadhaa zikiwaonesha Kiba na Tanasha wakiwa kimahaba zaidi, hali iliyozua gumzo hasa kwa wale ambao hawakuwahi kugundua kuwa mrembo huyo aliwahi kuwa ‘klozi’ na Kiba.

 

ZENGWE LA KIBA NA TANASHA

Kuibuka kwa zengwe la Kiba kudaiwa kutoka na Tanasha kumekuja kufuatia mwaka 2015 kuvuja picha za kimahaba za wawili hao bila kuwepo maelezo ya kueleweka kisha baadaye ikafahamika kuwa mrembo huyo alitumika kama video queen kwenye wimbo wa Kiba uitwao Nagharamia. Licha ya kubainika kuwa ilikuwa ni projekti, washakunaku wakaenda mbele zaidi na kusema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakiwapitia mavideo queen wao kisha ili kuziba soo wanasema wako kikazi zaidi.

PENZI LA TANASHA NA DIAMOND

Badaa ya Diamond kutangaza kujiweka kwa mwanadada huyo jumlajumla na kusema atamuoa soon, gumzo limekuwa kwamba; iweje achukue ‘makombo’ ya Kiba wakati amezungukwa na watoto wazuri wengi.

 

“Hivi Diamond ana maana gani kujiweka kwa demu ambaye bosi wetu alishapita, mbona kuna wasichana wengi wazuri? Hii ni kuonesha kuwa Kiba anaweza kuchagua ndiyo maana alipomuibua Tanasha kisha kumtosa, Diamond leo kamuona kifaa,” alisema Kilale Salum ‘Killer’ wa Sinza jijini Dar ambaye alijinasibu kuwa ni Team Kiba kindakindaki.

 

Wengine wameishia kuchukua picha za Diamond akiwa na Tanasha na zile za Kiba akiwa na Tanasha kisha kuuliza kuwa kapo ipi iko bomba ambapo ukifuatilia ‘comments’ utabaini mchuano mkali umekuwa kati ya Team Kiba na Team Diamond.

 

NI KWELI KIBA ALITOKA NA TANASHA?

Licha ya maelezo kwamba mastaa wengi wamekuwa wakitoka na mavideo queen wao kisha picha zao zikivuja wanasema ni projekti, baada ya hivi karibuni watu kudai kuwa Tanasha katoka na Kiba kisha sasa kahamia kwa Diamond, mrembo huyo alifunguka:

 

“Ningependa kufafanua tetesi ambazo zimekuwa zikiendelea kwenye kurasa mbalimbali za Instagram na blogs zinazonihusu mimi na Kiba. Niseme ukweli kabisa ni za uongo. Kiba na mimi tumefanya kazi pamoja, lakini kamwe hatujawahi kuwa wapenzi.”

AU DIAMOND NA TANASHA NI PROJEKTI PIA?

Wachambuzi wa maisha ya mastaa wamekuwa na mitizamo tofauti kuhusu penzi jipya la Diamond ambapo wapo wanaosema wawili hao wako siriasi lakini kuna ambao wanahitimisha kwa kusema kuwa, penzi lao limekaa ‘kiprojektiprojekti’.

 

“Najaribu kujiuliza kwamba, imekuwaje penzi hili liibuke kipindi hiki ambacho kuna Tamasha la Wasafi Festival na siyo kabla? Mimi kwa ninavyowajua hawa mastaa inaweza kuwa kuna projekti nyuma ya penzi hili. “Lakini hata kama ni projekti, kuna uwezekano Diamond akaungia humohumo kama alivyofanya kwa Zari, unakumbuka Zari na Diamond walianza kama ilivyokuwa Kiba na Tanasha lakini baadaye wakaungia humohumo na kuzaa.

 

“Sasa kama kwa Kiba na Tanasha iliishia kubaki projekti, kwa Diamond na Tanasha nako inaweza kuwa kuna projekti lakini tusije tukashangaa kweli wanaoana kama Diamond alivyojinasibu,” alisema Andrew Carlos, mwandishi wa habari za mastaa na burudani.

Madee Afunguka Babu Tale Kuwatosa TIP TOP Wasafi Festival

Loading...

Toa comment