The House of Favourite Newspapers

Kibadeni agomea mkataba JKT Ruvu, afundisha bure

0

KIBADENINEWQWKOCHA Abdallah Kibadeni anaifundisha JKT Ruvu bila mkataba malipo kwani sharti lake lilikuwa ni kuletewa Mrage Kabange awe msaidizi kwa kuwa ana majukumu mengine.

Kibadeni nyota na kocha wa zamani wa Simba, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, anataka kuitumikia JKT Ruvu pamoja na kituo chake cha kukuzia vipaji vya vijana cha Kibadeni Soccer Academy (Kisa), hivyo hataki abanwe.

“Nimekubali kuisaidia JKT, masuala ya fedha nimeweka kando ingawa sitakuwa na timu muda wote kwani nina majukumu mengine. Ndiyo maana niliomba niwe na Kabange kwa kuwa naujua vizuri utendaji wake,” alisema Kibadeni na kuongeza:

“Kuna muda (JKT Ruvu) watakuwa wanakuja kwenye akademi yangu kufanya mazoezi, maana kuna wachezaji wenye vipaji na sitaki vipotee.”

Kesho Jumapili itakuwa mtihani wa kwanza kwa Kibadeni ambapo ataiongoza JKT Ruvu dhidi ya Mwadui FC inayonolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.

Leave A Reply