The House of Favourite Newspapers

Kibadeni atamba Chalenji bila Samatta, Ulimwengu

0

KIBADENINEWQW.jpgKocha wa timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni.

Na Said Ally

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Abdallah Kibadeni, amesema ana uhakika kikosi chake kitafanya vizuri kwenye Kombe la Chalenji bila ya nyota Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Kilimanjaro Stars itacheza mechi yake ya kwanza kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Addis Ababa dhidi ya Somalia jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Samatta, Ulimwengu wa TP Mazembe ya DR Congo na kiungo Mrisho Ngassa wa Free State Stars ya Afrika Kusini, hawapo katika kikosi cha Kilimanjaro Stars na wamerejea katika klabu zao baada ya mchezo wa pili wa Taifa Stars na Algeria kufuzu Kombe la Dunia 2018.

Nyota wengi wa Taifa Stars, ndiyo wanaounda Kilimanjaro Stars na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.

Kibadeni aliliambia Championi Jumamosi: “Ni pengo kuwakosa Samatta, Ulimwengu na Ngassa, lakini nitajitahidi kuwatumia waliopo kuhakikisha tunapambana kupata ubingwa.”

Katika moja ya mechi za leo kwenye Uwanja wa Addis Ababa, Zanzibar Heroes iliyopo Kundi B itacheza na Burundi. Kesho katika Kundi B, Kenya itacheza na Uganda.

Kilimanjaro Stars ipo Kundi A sambamba na wenyeji Ethiopia, Somalia na Rwanda.

Leave A Reply