The House of Favourite Newspapers

Kiboko ya Okwi Apelekwa Yanga

0
Kikosi cha timu ya Prisons.

MABOSI wa Yanga wanaweza kucheka baada ya uongozi wa Prisons kusema upo tayari kuwauzia mshambuliaji wao Rashid Mohammed mwenye mabao sita ambaye anamkimbiza kwa ukaribu mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kwenye orodha ya wafungaji katika Ligi Kuu Bara.

 

Yanga wamekuwa wakimpigia hesabu mshambuliaji huyo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inamtegemea Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu, huku washambuliaji wengine wakiwa majeruhi.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha wa Prisons, Abdallah Mohammed ‘Bares’ amesema kuwa kama Yanga wana nia ya kumsajili mshambuliaji huyo, basi wao hawataweza kumzuia.

Emmanuel Okwi.

“Kama kweli Yanga wanamtaka mshambuliaji wetu, Rashid Mohammed basi sisi hatuna nia ya kumzuia badala yake tutawauzia tu, wanachotakiwa wao wafuate tu sheria za kumsajili ikiwemo kuja kuongea na uongozi. “Tukiwauzia, tutamuibua mshambuliaji mwingine kwa hata huyu ameonekana kuwa bora baada ya kupewa nafasi, hivyo hatuna wasiwasi kama akiondoka,” alisema Bares.

 

Taarifa ambazo Championi Jumatano, limezipata ni kuwa Rashid anaweza kutua Yanga kirahisi kutokana na mkataba wake na Prisons kumruhusu kwani umebaki miezi sita na sheria za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), linaruhusu mchezaji akibakisha miezi hiyo anaweza kuanza mazungumzo ya kujiunga na timu yoyote.

Stori: Said Ally, Championi Jumatano.

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

VIDEO: DK SHIKA KUWEKA HISTORIA USIKU WA 900 ITAPENDEZA

Leave A Reply