KIBOKO YA SANCHI AIBUKA, AONYWA

DAR: Kama ulikuwa bado unaamini kuwa mrembo mwenye figa matata pekee Bongo ni Sanchi, basi fahamu kuwa unakosea kuna mwingine anaitwa Scollah Wawuda ‘Binti Salim’ ambaye ameibuka kwenye tasnia ya uigizaji na kutikisa lakini hata hivyo wadau wamemuonya, Amani linakupa mchapo kamili.  

 

Msanii huyo ambaye ameanza kuuza sura kwenye ‘series’ ya Nanga inayorushwa kupitia Stars Times Swahili, amekuwa maarufu zaidi mitandaoni kutokana kuwa na umbo matata linalowadatisha zaidi wanaume.

 

Muigizaji wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ aliyeanza kuziona picha za msanii huyo kwenye mtandao wa Instagram alilieleza Amani kuwa, mrembo huyo amekuwa gumzo zaidi kwa sasa kiasi cha kumfunika Sanchi.

 

“Hili shepu ni kama lote. Ni zaidi ya lile la Sanchi maana kila mtu alikuwa akiamini Sanchi ndiye mwenye shepu la haja hususan katika saula zima la msambwanda, mtafuteni Global bwana mumuhoji,” alisema Dude.

 

Hata hivyo, Dude alimuonya Binti Salim kuwa makini asimuige Sanchi katika suala zima la picha za utupu kwani kwa sasa sheria ya makosa ya mtandao inafanya kazi na wasanii kibao wameshakutwa na panga la sheria hiyo.

“Tumeona ya akina Amber Rutty, tumeona akina Wema Sepetu, akianza na yeye kupiga za utupu itakula kwake maana mimi najua wasanii wenye maumbo kama yake huwa ni ngumu sana kuvaa mavazi ya stara,” alisema mdau huyo. Amani lilifanya jitihada za kumsaka mrembo huyo ambapo alipopatikana, alianza kwa kueleza historia yake kwa kusema kuwa yeye ni mtu anayejiheshimu.

 

“Najiheshimu kuliko hata watu wanavyodhani, hivyo kamwe siwezi kuvaa nguo ambazo hazina maadili, mimi ni mtu mzima na ninajitambua,” alisema Binti Salim. Akizungumzia maisha yake ndani ya sanaa, alisema alishawishiwa kuingia kwenye sanaa na rafiki yake aitwaye Hamisa na ndoto zake ni kuwa muigizaji mkubwa.

 

“Ndoto yangu ni kuwa muigizaji mkubwa lakini pia kujiendeleza kibiashara maana tayari ninafanya biashara ya kununua vitu mbalimbali Kariakoo na kupeleka mkoani,” alisema na kuongeza: “Namshukuru Mungu tayari nimeanza kuonekana kupitia series ya Nanga Star Times na pia nategemea kucheza filamu nyingi tu.”

 

Alipoulizwa kuhusu usumbufu anaoupata kutoka kwa wanaume wakware ambao wanavutiwa na picha zake mitandaoni na mitaani alisema hilo ni jambo la kawaida kwake lakini kikubwa ni kwamba anajiheshimu. “Nina mtu wangu mmoja tu, najiheshimu hivyo siwezi kujirahisisha. Usumbufu upo sana tu, lakini binafsi najiheshimu na ninampenda mpenzi wangu siwezi kumsaliti.” Alisema Binti Salim’.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Toa comment