The House of Favourite Newspapers

Kicheko kilio ni sehemu ya mapenzi

0

sex-habits-of-super-happy-couplesMpenzi msomaji wangu, napenda kukukaribisha sana katika safu yetu ya XXLove kama kawaida. Jumatatu hii tutajifunza mambo mawili muhimu katika uhusiano wa kimapenzi na maisha ya kawaida. Mambo hayo ni kicheko na kilio ambavyo mwanamke au mwanaume hupaswa kufahamu kuwa ni sehemu ya mapenzi.

Kama ulikuwa haujui au hujaweka akilini mwako, basi leo ufahamu na uliweke hili akilini mwako kuwa maisha ya mwanadamu yamegawanyika katika sehemu kuu hizo mbili.

KILIO AU MAJONZI
Hii ni moja ya sehemu muhimu katika maisha yako ya kila siku, uwe mwanaume au mwanamke, kilio au majonzi yapo kwa watu wa rika, tabia, uwezo, nyadhifa, elimu, rangi na jinsi zote.

NINACHOMAANISHA
Kuna siku mwenza wako anaweza kuamka vibaya, wengi tunaufahamu msemo usemao ‘siku njema huonekana alfajiri’. Msemo huo unaweza kujidhihirisha katika maisha yetu ya kawaida na hata kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Kama siku njema imeanza vibaya kwa mwenza wako, kwa kukwazwa au kumkwaza, ukimuuliza kitu mwenza wako unajibiwa kwa kifupi bila tabasamu wala ushirikiano kwa lolote. Ukiomba kuletewa kitu hauletewi ila unaoneshwa kilipo ili ukachukue mwenyewe.

Hata sura ya mwenza wako ukiiangalia unaiona kabisa imejaa mikunjo ya hasira, basi ujue mpenzi wako hayuko sawa.Ukishafahamu mazingira hayo na mengine mengi, basi jifunze namna ya kuishi naye kwa siku hiyo ili kuimaliza siku vizuri bila kuingia kwenye mgogoro au zaidi ya hilo.

WAKATI MWINGINE
Wakati mwingine inawezekana wewe mwanaume au mwanamke ndiyo chanzo cha majonzi au mateso ya mwenza wako kwa kufahamu au kutokufahamu.

Kama umekwazika kwa sababu ya mpenzi wako ni jambo la busara na hekima sana kama ukimwambia kiuungwana kosa au kitu kilichokufanya ukajikuta ukiingia katika majonzi au kilio kuliko kugugumia na maumivu wakati huo aliyesababisha ana furaha tele moyoni mwake.

EPUKA
Jenga uwezo wa kutatua mwenyewe na mwenza wako matatizo yenu na kama ikishindikana, tafuta mtu mmoja mwaminifu na mwenye busara ili kuweza kukusaidia kumaliza matatizo yenu.

Tukutane wiki ijayo kwenye mwendelezo wa mada hii. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook na Instagram.

Leave A Reply