The House of Favourite Newspapers

Kichuya Atoa Tamko Zito Simba

Shiza Kichuya.

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amewaambia mashabiki kwamba mechi ya Jumapili dhidi ya Stand United ni muhimu kuliko hata zote walizocheza tangu msimu uanze. Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa huku mashabiki bado wakiwa na simanzi la kutekwa kwa muwekezaji wao, Mohammed Dewji ‘MO’.

 

“Mechi yetu na Stand ni muhimu kuliko hata zile tulizocheza tangu ligi ianze.

 

Yaani tunahitaji ushindi na furaha, siku zote huwa inakuja tunapopata ushindi hivyo natarajia ushindi mkubwa mechi hiyo,”alisisitiza Kichuya ambaye anaonekana kupania sana ili kuweka hali ya mambo sawa ndani ya Simba.

 

“Nimekuwa na uhaba wa magoli msimu huu ila karamu ya kufunga naianzia kwa Stand United ili kurejesha ubora wangu wa siku zote na kuwaonyesha mashabiki wa Simba kuwa bado nipo vizuri katika kufumania nyavu kama ilivyokuwa msimu uliopita,”alisema Kichuya ambaye ni mwenyeji wa Morogoro.

 

Msimu uliopita Kichuya alifunga mabao saba na asisti za kumwaga zilizoipa Simba ubingwa. Msimu huu amefunga bao moja katika michezo yote aliyocheza mpaka sasa.

STORI: ADRIAN MAYUNGA | CHAMPIONI

Comments are closed.