KICHUYA AZIPIGIA HESABU PRISONS, YANGA

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, amesema matokeo ya mechi yao dhidi ya Tanzania Prisons leo Jumatatu, ndiyo yataamua ubingwa wao Bara huku wakimaliza kazi dhidi ya watani wao Yanga.

Simba inatarajia kuku­tana na Prisons leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Simba ambayo inaon­goza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 55, kama ikishinda leo itaku­wa imeiacha Yanga kwa tofauti ya pointi 11 lakini Yanga ikiwa na michezo miwili mkononi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kichuya alisema kuwa mechi yao na Prisons ndiyo itakayoamua ubingwa wa Simba kwa kuhakikisha wanashinda mchezo huo kwa hali na mali.

 

“Mechi yetu na Prisons ndiyo itakayoamua ub­ingwa wetu msimu huu tukifanikiwa kuwaumiza wao tutakuwa tumeji­weka katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa.

“Tukimaliza mechi hiyo tunaangalia mechi ya wale wenzetu wa upande wa pili, tuna­hakikisha tunawafunga ili tunyakue ubingwa rasmi,” alisema Kichuya

Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment