Kidato cha Tatu Anaswa Ubakaji kwa Ubakaji wa Denti Mwenzake!

MOROGORO: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia denti wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Mji Mpya akidaiwa kumbaka denti mwenziye wa kike na kumsababishia atokwe na damu nyingi na kupoteza fahamu.

 

Tukio hilo lililojaza umati wa watu limetokea Jumamosi iliyopita majira ya mchana Kata ya Mji mpya mkoani Morogoro. Taarifa zinadai kuwa baada ya denti huyo kudaiwa kumbaka mwenzake alishtuka kuona denti huyo anavuja damu nyingi isivyo kawaida, hivyo akaamua kumkimbizia katika Kituo cha Afya cha Kata ya Mji Mpya.

 

Inadaiwa kwamba baada ya kufika hapo na kutoa maelezo, wauguzi walimtaka denti huyo wa kiume kwenda kuchukua PF3 kituo cha polisi na kwamba baada ya kuelezwa hivyo alikurupuka na kutimua mbio.

Hata hivyo, kundi la wananchi wengi wao wakiwa ni wapiga debe wa stendi ya daladala ya Mji Mpya Kaloleni iliyopo jirani kabisa na zahanati hiyo walifanikiwa kumkamata na kumpeleka Kituo cha Polisi, Kata ya Mji mpya kilichopo pia jirani na zahanati hiyo.

 

Baadhi ya wananchi waliamua kutoa taarifa kwa Kamanda wa Operesheni Fichua Maovu (OFM) Mkoa wa Morogoro ambaye ndani ya dakika sifuri alitinga eneo la tukio.

Mara baada ya kufia eneo hilo, kamanda huyo alishuhudia denti huyo wa kike akipandishwa kwenye gari la wagonjwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kutokana na hali yake kuwa mbaya hivyo kupewa rufaa.

 

Baada ya hapo mwandishi wetu alitinga Kituo cha Polisi Mji Mpya na kushuhudia pia denti huyo wa kiume naye akitolewa ndani ya kituo hicho na kupelekwa kituo kikuu cha polisi kutokana na ukubwa wa kosa analotuhumiwa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Fumilwa B, Kata ya Mji Mpya, Said Fungu aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake akiwa kituo cha polisi na alikuwa na haya ya kusema.

 

“Kweli kuna tuhuma za kijana huyu kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Mji Mpya.

“Inadaiwa baada ya kitendo hicho aliona mwenzake anatokwa na damu nyingi akaamua kumpeleka zahanati, sasa alipotakiwa kuja hapa polisi akakimbia lakini akakamatwa na wananchi tukamleta hapa kituoni.

“Muda huu tumekodi gari na tumembeba mzobemzobe mtuhumiwa na tunampeleka kituo kikuu cha polisi.”

 

Akizungumza na gazeti hili la Amani, baba wa denti huyo wa kike aliyefahamika kwa jina la Niger Kobelo Jongo alikuwa na haya yakusema:

“Huyu binti ni mtoto wa marehemu kaka yangu na mimi ndio namlea.

“Nasikia huyo denti aliyefanya tukio hili alikuwa anamtongoza kwa muda mrefu na siku ya tukio (Jumamosi iliyopita) akiwa na mwenzake walitumia njia kama ya kumteka binti yangu mpaka kwenye geto lao.

 

“Walipofika yakatokea haya ya ubakaji, binti anasema alizibwa mdomo huku akimbaka kisha akawa anavuja damu nyingi.

“Baada ya kuona anavuja damu nyingi kijana anayetuhumiwa akaamua ampekeke hospitali. Hivi ninavyoongea na wewe binti yangu bado amelazwa na hali yake sio nzuri.

“Muda huu nimeitwa polisi kituo kikuu kama mzazi, nimetoa maelezo yangu kisha nikapewa namba ya kesi MOR/RB/6690/2019 (UBAKAJI).

 

“Cha ajabu hii ni kesi ya ubakaji haina dhamana, huyo mpelelezi wa kesi yangu amewaambia ndugu wa huyo mtuhumiwa kwamba dhamana iko wazi ili hali bado mwanangu amelazwa hospitali.”

Afisa mmoja wa polisi ambaye amedai siyo msemaji amethibitisha kukamatwa kwa kijana huyo na amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

Stori: Dunstan Shekidele, Amani

Loading...

Toa comment