The House of Favourite Newspapers

Kidoa aachana na ufuska

0

KIDOA-61MAYASA MARIWATA, AMANI

MODO mwenye figa matata Bongo Asha Salum ‘Kidoa’ amesema kuwa, ameamua kutulia kuachana na maisha ya ufuska baada ya kupigwa marufuku na mwandani wake ambaye ni kigogo wa serikali anayemuweka mjini.

Akipiga stori na Showbiz Xtra Kidoa alisema, amejikuta kwenye wakati mgumu kwa kuwa kuna vitu vingi vya ujana amelazimika kuachana navyo vikiwemo mambo ya ufuska na skendo kwa sababu ya kulinda penzi lake hilo, ambalo ndugu wa pande zote wameshalibariki.

“Mwanaume wangu ambaye ndiyo naishi naye na nina malengo naye amenipiga marufuku mambo ya ajabuajabu, yaani ananifuatilia kila kona kuanzia marafiki ninao kuwa nao, mambo ya skendo hadi mitandaoni nipo makini sana nisije vunja uchumba, hivyo nimeamua kutulia nisimkwaze,” alisema.

Leave A Reply