Kidoa Afunguka Kuwa Mke Bora, Awashangaa Wanaume!

WAOAJI mpo? Video queen ambaye kwa sasa amegeukia kwenye uigizaji Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’
amefunguka kuwa yeye ni ‘waifu matirio’ (mke bora) hivyo anashangaa kwa nini wanaume hawamuoni.

 

Kidoa ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, anajijua yeye ni miongoni mwa wanawake wanaostahili kuwekwa ndani kwa sababu anajiamini kwenye tabia na kila kitu.

“Unajua ukiwa msanii, mtu anaweza kukufikiria kuwa huwezi kuwa mke bora, lakini ukweli ni kwamba ninastaili kuwa mke bora wa kuwekwa ndani na nikatulia kabisa,” alisema Kidoa.


Loading...

Toa comment