Kidoa Asaka Maisha China, Aahidi Kuwahudumia Mashabiki Wake

Mwigizaji maarufu wa filamu za Bongo Muvi, Asha Salum almaarufu Kidoa, ameendelea kuonyesha jitihada za kujiongezea kipato kwa njia mbalimbali, safari hii akiwa China, ambako ameenda kusaka bidhaa mbalimbali za watoto na mahitaji mengine kwa ajili ya biashara.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kidoa amewaambia mashabiki na wateja wake kuwa yuko tayari kutumiwa kwa mahitaji mbalimbali kutoka China hadi nyumbani kwa gharama nafuu.
“Wale Tajiri zangu mlionituma mzigo unawafikia soon😉… Nitume Tajiri, nipo tayari kuwahudumia,” aliandika Kidoa kwa furaha.
Hatua hii ya Kidoa imeibua mjadala mtandaoni, wengi wakimpongeza kwa ubunifu na juhudi za kutafuta kipato nje ya sanaa ya uigizaji.