visa

Kidoa Mjamzito?

BAADA ya kudaiwa ni mjamzito kwa sasa, mwanadada Asha Salum ‘Kidoa’ ambaye alijipatia umaarufu kupitia uvideo queen na sasa amegeukia kwenye filamu, ameibuka na kufungukia ishu hiyo.

Sema kuna watu wengi wanajua yeye ni mjamzito, lakini sio inawezekana tu tumbo limeongezeka.

Akipiga stori na Amani, Kidoa ambaye kwa hivi sasa yupo nchini Afrika Kusini akila bata, alisema watu wengi wamekuwa wakisema ana ujauzito lakini siyo kweli ila amenenepa tu na tumbo kuonekana kubwa lakini siyo vinginevyo.

“Watu wengi nikikutana nao wanasema kuwa nina ujauzito, lakini ukweli ni kwamba sina. Bado nakula zangu bata tu huku Afrika Kusini ili nipunguze ‘stress’,” alisema Kidoa kwa njia ya Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp alipoulizwa na Amani kuhusu habari hizo.
Toa comment