Kiduku Achezea Kichapo Kutoka Kwa bondia wa Ujerumani Juergen – (Picha + Video)
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini anayepigana kwenye uzito wa Super Welter, Twaha Kassim ‘Kiduku’, usiku wa kuamkia Oktoba 1, 2024 amepoteza pambano lake dhidi ya bondia wa Ujerumani Juergen Doberstein kwa pointi lililochezwa usiku wa kuamkia jana nchini Ujerumani.
Pambano hilo la uzito wa kati lilipigwa ukumbi wa Jo Deckarm Halle, katika mji wa Saarbruecken nchini Ujerumani.
Kiduku alipoteza kwa pointi za majaji watatu ambao ni Iwan Horn, Nikita Horn na Ruslan Svider waliotoa pointi kwa Doberstein 120-107, 120-107 na 119-108.
Kupoteza kwa Kiduku kumempandisha hadhi Mjerumani huyo na kuwa na nyota mbili na nusu. Kabla ya pambano hilo alikuwa na nyota mbili sawa na Kiduku.
Hilo ni pambano la 10 anapoteza Kiduku katika ngumi za kulipwa, lakini bado ana rekodi nzuri katika ushindi wa mapambano 24 na sare moja kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa ngumi za boxrec.