Kieran Gibbs Aingia Kwenye Skendo ya Usaliti

NAMKUMBUKA beki wa pembeni Kieran Gibbs ambaye aliwahi kukipiga Arsenal? Sasa baada ya kupotea kwa muda mrefu, hivi karibuni ameibuliwa na skendo ya kutembea na mpenzi wa mchezaji wa mpira wa kikapu.

 

Mrembo India Reynolds inadaiwa kuwa alimsaliti mpenzi wake Ovie Soko kwa kujihusisha kimapenzi na Gibbs, 29, ambaye siku hizi anaichezea West Bromwich Albion inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza England (Championship).

 

Hata hivyo, mwanamitindo huyo, 28, amekanusha taarifa hizo akidai ana mahaba mazito kwa Ovie.

Skendo ya India kujihusisha kimapenzi na Gibbs iliibuka baada ya mrembo huyo kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mwanasoka huyo nchini Ureno.

 

Gibbs alisaini West Brom mkataba wa miaka minne mwaka 2017 akitokea Arsenal akaichezea timu hiyo kwenye Premier msimu wa 2017/18 kabla ya kuporomoka nayo daraja msimu huo na kucheza Championship hadi sasa.

BREAKING: RAIS MAGUFULI AMTUMBUA DC NA DED WA MALINYI


Loading...

Toa comment