The House of Favourite Newspapers

Kifo cha Filikunjombe, mapya yaibuka

0

maxresdefault

Marehemu Deogratius Haule Filikunjombe ‘Deo’ enzi za uhai wake.

Na Waandishi Wetu
NI mapya! Ni kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), marehemu Deogratius Haule Filikunjombe ‘Deo’ (43) kilichotokea Oktoba 15, mwaka huu kwenye Hifadhi ya Wanyama ya Selous kwa kuanguka na helikopta, mapya yameibuka, moja ikidaiwa kuwa, kumbe Deo aliruka kabla ya chombo hicho kufika chini.

IMG_5481Majeneza yaliyobeba miili ya marehemu yakiandaliwa kwa ajili ya kuagwa.

Katika ajali hiyo, mbali na Deo, wengine waliopoteza maisha ni rubani wa helikopta hiyo, Kapteni William Slaa, Plasdus Ngabuma Haule (53) na Egid Francis Nkwera (43).

APYA YALIYOIBUKA
Baada ya ajali hiyo kutokea Alhamisi, siku ya Ijumaa, Uwazi lilifanikiwa kufika eneo la tukio wakati uokozi wa miili ya marehemu, hususan wale walioteketea kabisa kwa moto, ukiendelea.

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo ambao ni askari wa mbuga hiyo walisema wanachokijua wao ni kwamba, wakati helikopta inashuka chini kwa kasi huku ikiwa inawaka moto, marehemu Deo aliruka.

SIKIA SIMULIZI YA MACHOZI
“Sisi tulifika hapa na kukuta wote wameshapoteza maisha, lakini kulikuwa na tofauti kubwa ya hali za miili yao. Mwili wa Deo na wenzake ilipishana katika kuungua. Wenzake waliteketea mpaka kubaki mkaa, yeye aliungua kwa kubabuka mwili mzima.”
HALI YA MWILI WA DEO
“Mwili wa Deo tuliukuta ukiwa umejikunja. Mikono ilikuwa inaangalia pembeni, kama aliitanua. Deo aliruka kutoka kwenye helikopta, hilo halina ubishi.”
Uwazi: “Mlijuaje kama Deo aliruka?”

Shuhuda: “Tulimkuta miguu yake imevunjika. Hii ni ishara kwamba aliruka kabla helikopta haijafika chini. Pia mahali tulipoukuta mwili wake na mahali ilipoangukia helikopta na wenzake si moja. Inaonekana kuwa yeye baada ya kuruka alijitahidi kujiokoa kutoka sehemu aliyoangukia ili kuukimbia moto uliowaka baada ya helikopta nayo kuanguka.

IMG_1273

Mke wa marehemu akiwa mwenye simanzi kubwa.

“Mahali alipoangukia Deo na mahali ilipoangukia helikopta na wenzake ni kama umbali wa mita tano. Kwa hiyo Deo aliungua kwa kubabuka kutokana na moto uliyoiteketeza ile helikopta.”

ALIJITAHIDI KUJIOKOA
“Ukiangalia mwili wake tulivyoukuta, inaonekana baada ya kuanguka, alijitahidi kujiokoa kutoka eneo lile ambalo moto ulikuwa ukiwaka lakini akashindwa kwa sababu miguu ilikuwa haifanyi kazi kwa kuvunjika. Deo alishindwa kutembea.”

MOTO ANGANI
Mmoja wa askari hao alisema kuwa, yeye alianza kusikia mlio wa helikopta angani. Alikaza macho kuangalia. Lakini ghafla akaona chombo hicho kinawaka moto na kisha kuanza kushuka chini kwa kasi.

HABARI ZASAMBAA, SIMU YAKE YAITA
Cha ajabu, wakati mitandao mbalimbali ya kijamii usiku wa Alhamisi ikitoa taarifa tata za kuanguka kwa helikopta hiyo yenye namba 5 Y-DKK, baadhi ya watu wake wa karibu waliipiga simu ya Deo ambayo iliita bila kupokelewa.

IMG_1268

Mke wa marehemu akienda kuaga mwili wa mumewe.

“Hata mimi nakubali Deo aliruka ndiyo maana simu yake ilikuwa hewani, maana wale wenzake mpaka helikopta inafika ardhini, wote walikuwa ndani na kuungua palepale. Kwa kuwa Deo aliruka akatua pembeni, ndiyo maana simu yake ilikuwa hewani. Lakini baadaye ikazima, pengine iliisha chaja au joto kali la moto,” alisema mmoja wa watu wa karibu na marehemu huyo.

SHABIBY NAYE ANENA YAKE
Ahmed Mabkhut Shabiby ni mgombea ubunge Jimbo la Gairo kwa ‘leseni’ ya CCM. Yeye anaitolea ushuhuda helikopta iliyopoteza maisha ya Deo akisema kuwa, haamini kama chombo hicho kilipata hitilafu angani kwa vile amewahi kuitumia na anajua ilikuwa vizuri.

Anasema: “Mimi nimeshaitumia mara kadhaa ile helikopta tena kwenye Milima ya Udzungwa. Nikisema Milima ya Udzungwa, wanaoielewa wanajua namaanisha nini. Sikuwahi kuona kwamba helikopta ile ina matatizo.

Avoq_xl5YFXql_P8DxHoO3ML4oEJtmRnnrsu4mk57mho“Yule rubani wake (marehemu Slaa) alikuwa mzoefu sana. Anajua analolifanya. Mimi nimeshangaa sana. Bado sijaamini.”

VILIO VYATAWALA DAR, LUDEWA
Wakati mapya yakiwa hayo, simanzi na vilio viliendelea kutawala nyumbani kwa marehemu huyo, Kijichi Dar wakati miili ya marehemu ikiwasili kutoka Hospitali ya Jeshi Lugalo na Ludewa mkoani Njombe wakati wa mazishi.

Miili ya marehemu watatu, ilisafirishwa pamoja Jumamosi iliyopita kwenda Ludewa kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika juzi kwenye Makaburi ya Kanisa la Romani Katoliki, Njemba.

Ajuv6ihn3-MQ2wjplu8xwOn8DnxmbzGqNaw9quuAhhtS1

Mwili wa aliyekuwa rubani wa helikopta hiyo ambaye pia ni baba mzazi wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake, Jerry Slaa uliagwa nyumbani kwake Gongo la Mboto, Ilala, Dar na kuzikwa Oktoba 18, mwaka huu katika Makaburi ya Pugu.

HIFADHI YA SELOUS
Hifadhi ya Selous ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote nchini Tanzania. Pia ni kati ya hifadhi kubwa kwa wanyama duniani. Eneo lake ni kilomota za mraba 54,600.

Ipo katika Mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Ndani ya hifadhi hiyo wanapatikana wanyama kama tembo, faru, simba, twiga, viboko na mamba, hali ambayo baadhi ya askari wanasema pia ingekuwa vigumu kwa Deo kusalimika na wanyama hao kama angetoka majeruhi na kutembea kutafuta mji.
Stori: Makongoro Oging’, Haruni Sanchawa na Francis Godwin.

Leave A Reply