The House of Favourite Newspapers

Kifo cha Mama… Dogo Janja, Mkewe Uwoya Wampa Nguvu Johari – Video

Uwoya akizungumza naGlobal TV Online.

SO SAD! Kufuatia kifo cha mama mzazi wa Staa wa Bongo Movies, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’, Bi. Asha Chagula, maeneo ya Mburahati, jijini Dar wasanii wenzake Dogo Janja na mkewe Irene Uwoya jana walipata fursa ya kumtia moyo na kumpa nguvu ambapo walimtaka asikate tamaa na achukulie ni hali ya kawaida inayoweza kumtokea binadamu yeyote, wakati wowote.

 

Wakizungumza na Global TV Online baada ya mazishi hayo jana Alhamisi katika Makaburi ya Kisutu, Dogo Janja alisema;

“Taarifa tulizipata mapema alfajiri mimi na mke wangu, na tangu msiba utokee tumekuwa karibu nafamilia tukifarijiana. Anachokihitaji Johari kwa sasa ni faraja, tutaendelea kumfariji hadi pale atakaporudi kwenye hali yake ya kawaida.

 

Naye Uwoya akazungumza;

“Taarifa za mama kuugua nilikuwa nazo, alikuwa akisumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu. Nachoweza kumshauri Johari ni kuwa mvumilivu, mama ametangulia na sisi tutafuata, hakuna mtu atakayekwepa, kikubwa ni kujipa moyo na kumuombea mama apumzike kwa amani. Ana wadogo zake wanamtegemea hivyo asivunjike moyo.”

 

VIDEO: DOGO JANJA NA MKEWE UWOYA WATOA NENO MSIBA WA MAMA WA JOHARI

Comments are closed.