The House of Favourite Newspapers

Kifo cha Mke wa Babu Tale, Harmonize ‘Ahukumiwa’

0

ULE msemo usihukumu, usije ukahukumiwa umetokea kwenye msiba wa mke wa Hamis Tale ‘Babu Tale’, Shamsa Kombo.

 

Jicho la mwandishi wetu kwenye mitandao ya kijamii lilibaini kuwa bosi wa Lebo ya Konde Gang Music WorldWide, Rajab Abdul ‘Harmo’, alihukumiwa vilivyo na baadhi ya watu kwa kile kilichotajwa kuwa, ni kushindwa kuposti chochote kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii juu ya msiba huo, jambo ambalo lilitafsiri kuwa ni kutokujali.

 

Wakati tafsiri hiyo mbaya ikienezwa kwenye mitandao ya kijamii ikiambatana na komenti zenye lugha chafu kwa msanii huyo, ghafla Harmo aliibuka msibani mkoani Morogoro na kuzua gumzo.

 

“Jamani si walisema Harmo hajali msiba wa mke wa meneja wake wa zamani, mbona kaenda msibani?” mtu mmoja aliandika komenti yake kwenye ukurasa wa Instagram baada ya picha ya msanii huyo akiwa msibani kupostiwa.

 

HARMO ALIVYOTAFSIRIWA

Saa chache baada ya kutokea kwa kifo cha mke wa Babu Tale, ambapo mastaa wengi walitumia mitandao ya kijamii kumpa pole mfiwa, kwa Harmo haikuwa hivyo kwani hakuposti chochote kinachohusu msiba na hivyo kutafsiriwa na wengi kuwa ni mtu mwenye roho mbaya.Ifahamike kuwa Babu Tale ni meneja wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’ ambayo ndiyo imekuza kipaji cha Harmo kabla hajaihama.

KOMENTI ZA KUMSHAMBULIA HARMO

“Kuna watu hawana shukrani duniani jamani, kwa lipi baya alilomfanyia Babu Tale hadi ashindwe kumpa pole?”

“Ni roho mbaya na kusema kweli hana utu, mimi kwa hili nimemchukia.”

“Uhasimu wa muziki hadi kwenye misiba, shame on you Harmonize.”

Hivyo ndivyo baadhi ya komenti kwenye mitandao ya kijamii zilisomeka kuonesha mashambulizi ya wazi kwa Harmo baada ya wenye macho yao kutoona pole yake kwa bosi wake wa zamani.

 

WATAWAAMBIA NINI WATU

Hata hivyo, katika hali ya kuwatahayarisha nyuso zao waliomlaumu, Harmo aliambatana na wafiwa kuusafirisha mwili wa marehemu Shamsa hadi Morogoro ambako pia alishiriki maziko yake.

Kitendo hicho kiliwafanya waliomsema vibaya kutafuta pa kuficha sura zao kutokana na hukumu zao za mapema walizomhukumu msanii huyo.

“Mtaweka wapi sura zenu ninyi watu, mara ooooh ana roho mbaya, kanuna mara…sasa kiko wapi?“Majitu mengine kazi yao kulaumu tu kila jambo bila hata kupima ukweli, sasa Harmo awafanye nini mliompakazia ujinga?”

“Myakalie yawanukie, maana jamaa kachana mkeka wenu.”Hizi ni baadhi ya komenti kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambazo jicho la mwandishi wetu liliziona baada ya Harmo kuibuka msibani Morogoro.

 

ALI KIBA APONGEZWA

Licha ya wengi kuandika hisia zao juu ya kifo cha mke wa Babu Tale kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii, mtu aliyewafurahisha wengi ni msanii hasimu wa WCB, Ali Kiba ambaye aliweza kuonesha masikitiko yake juu ya kifo cha mke wa Babu Tale kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliwapa pole wafiwa na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

 

“Muziki ni muziki na msiba ni msiba, hongera Kiba kwa kujali msiba wa Wasafi,” mmoja kati ya komenti iliyompongeza Kiba.

 

KIFO CHA SHAMSA CHAUMIZA WENGI

Katika hali ambayo inaonesha kuwa Shamsa au wengi walimuita ‘Shammy’, alikuwa mtu wa watu, wengi wameumizwa na kifo chake na kujitokeza kwa namna moja au nyingine kushiriki msiba wake.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo aliandika ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Instagram kuonesha kuguswa vilivyo na kifo cha mwanamke huyo aliyeacha watoto watatu.

“Shammy tarehe 11.06.2020, ulinitumia huu, ujumbe wa simu- Buriani. Nilelee wanangu!

“Nilishtuka kupata huu ujumbe kutoka kwako. Sikuelewa. Leo bado sielewi. Ila nitajitahidi kufanya kama ulivyoniomba. Nilikupenda, nilikuheshimu kwa sababu ulikuwa mtu mwema sana na muungwana sana,” aliandika Jokate.

Shammy alifariki dunia, Jumapili na mwili wake kusafirishwa hadi Mkuyuni mkoani Morogoro ambapo ulizikwa Juni 29.

Leave A Reply