The House of Favourite Newspapers

Kigogo amjengea mjengo Vai wa Ukweli!

0

VaiwaUkweliMuigizaji Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’

NA MWANDISHI WETU, RISASI MCHANGANYIKO

DAR ES SALAAM:

Licha ya madai kuwa soko la ­ lamu Bongo limeshuka na hivyo kutokuwa na faida kwa wasanii, uigizaji Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ anadaiwa kujengewa nyumba na kigogo anayetajwa kuwa ni mfanyabiashara, maeneo ya Mbezi-Msumi, jijini Dar. Chanzo cha uhakika kililiambia gazeti hili kwamba Vai wa Ukweli tangu awe na kigogo huyo maisha yake yamebadilika kwani muda mwingi anakuwa bize na kusimamia ujenzi wa nyumba yake hiyo ambayo hivi sasa ime­ kia usawa na madirisha.

“Vai yuko vizuri sana sasa hivi, maana muda mwingi anakuwa kwenye nyumba yake hiyo akiwasimamia mafundi kwa hiyo zile tabia za kupiga misele kwenye viwanja mbalimbali vya starehe siku hizi zimepungua.

“Kuna habari kwamba anajengewa na kigogo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa madini hapa mjini maana si unajua ­ lamu hazilipi na yeye mwenyewe hana kazi nyingine ya maana anayofanya,?” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Vai wa Ukweli na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, ambapo alijitetea kama ifuatavyo;

“Jamani ni kweli ninajenga lakini sijengewi na mtu yeyote, watu waache umbeya, najenga kwa hela yangu mwenyewe ambayo nimeipata kwenye ­ lamu na nyingine kwenye biashara zangu nyingine.”

Hata hivyo, licha ya gazeti hili kutaka kufahamu kuhusu ‘biashara zake zingine’ ni zipi, muigizaji huyo alipotezea bila kutoa ufafanuzi.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply