The House of Favourite Newspapers

Kigogo anayempa jeuri ya pesa Uwoya Huyu Hapa!

BAADA ya swali la wapi anapo­toa jeuri ya fedha muigizaji Irene Uwoya kugonga vichwa vya watu wengi kwa muda mrefu, hatimaye siri imefichuka baada ya Ijumaa Wikienda kuelezwa mhusika!

 

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kipo karibu na msanii huyo, jeuri hiyo anaipata kutoka kwa kigogo mzito aliyepo kwenye Serikali ya Kenya.

“Ni kigogo (anamtaja jina, tunalihifadhi sababu hatujam­pata kuthibitisha) katika Seri­kali ya Kenya, ndiye ambaye anamuwezesha kwa kila kitu. Hizi sijui kufuru za bethidei yake, sijui kujiachia kwenye boti hadi Zanzibar kigogo huyo ndiye anayemuweze­sha,” kilidai chanzo hicho.

 

Chanzo hicho makini kilizidi kwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa, kutokana na uzito wa kigogo huyo, imekuwa ngumu kujulikana na hata anayejua pia huhofia kusema.

“Ni kutokana tu na uzito wa kigogo huyo na bahati mbaya sana ni kwa sababu yupo Kenya, ingekuwa yupo Bongo ingekuwa ni rahisi sana watu kumjua,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:

 

“Kigogo huyo ndiye anayed­hamini pia zile safari za mara kwa mara za Uwoya nchini Dubai, nafikiri huwa wanaku­tania huko na huyo kigogo kula zao raha.”

Baada ya gazeti hili kupata habari hiyo lilimtafuta Uwoya na kumuuliza kuhusiana na madai hayo ambapo alifun­guka kama ifuatavyo:

 

Ijumaa Wikienda: Hebu tu­weke wazi, tumeelezwa kuwa jeuri uliyonayo ya fedha kwa sasa hivi unapewa na kigogo wa serikalini nchini Kenya (anatajiwa jina la kigogo) je ni kweli?

Uwoya: (Kicheko) Hivi kwa nini kila mtu anapenda kumjua mtu wangu maana marafiki wanapenda kumjua, wasanii wenzangu, mpaka ndugu zangu yaani watu wa­nahangaika kweli jamani.

Ijumaa Wikienda: Sawa ila tunataka kufahamu ukweli ni upi?

 

Uwoya: Huyo (anamtaja jina) nampenda sana labda niseme hivyo, siku akija Bon­go watu watafunga midomo yao.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo unatuthibitishia kuwa ni mpenzi wako au vipi?

Uwoya: Mtajua muda mua­faka ukifika na hata akiwa sio pia mtajua baadaye.

Siku za hivi karibuni, Uwoya amekuwa akiponda raha na kundi la mastaa wenzake katika viunga mbalimbali vya starehe huku ikielezwa yeye ndiye anayesimamia mpango mzima wa starehe, hivyo watu wengi kuhoji aliyeko nyuma yake.

Stori: Imelda Mtema,Dar

Comments are closed.