The House of Favourite Newspapers

Kigogo Atajwa Mjengo wa Mobeto

0

DAR: MJINI utanyimwa chakula lakini umbea utaupata bure, Mrembo Hamisa Mobeto amevumishiwa skendo kwamba mjengo mpya ‘aliyojimwambafai’ kuhamia hivi karibuni amepangishiwa na kigogo mmoja aliyepo serikalini. 

 

Mwanzo Mobeto alidaiwa kuwa mjengo huo uliopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ni wake, baadaye ikavuja ishu kwamba amepanga lakini chanzo chetu kimesema taarifa zote hizo ni za uongo kwa madai kwamba si mjengo wake wala hajapanga kwa fedha yake mwenyewe ila kapangishiwa na mwanaume.

 

“Kuna mtu mzito serikalini (cheo na jina linahifadhiwa) ndiyo kampangishia hiyo nyumba,” chanzo kilisema bila kufafanua huyo mwanaume ana uhusiano gani na Mobeto.

 

Mapema wiki iliyopita, picha za mjengo huo wa ghorofa zilivuja kupitia kurasa za wapambe wa Mobeto katika mtandao wa Instagram na kuibua mjadala mkubwa ambao mpaka sasa umezidi kuleta sintofahamu.

Mwandishi wetu alimtafuta Mobeto kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi kuhusu nyumba hiyo lakini hakupatikana na alipomtafuta mama yake mzazi aitwaye Shufaa Rutiginga, alipomuuliza kinachosemwa kwenye mitandao ya kijamii, alisikiliza swali na kisha kukata simu bila kutoa majibu.

 

Mara nyingi kauli za mama Mobeto kuhusiana na mwanaye zimekuwa zikipishana na zile za mtoto wake ambapo hivi karibuni Mobeto aliibuka na hoja ya kuzawadiwa gari na mtu katika siku yake ya kuzaliwa lakini mama yake alipoulizwa alisema mwanaye kajizawadia na hivyo kusababisha mgongano wa kauli.

 

Hata hivyo, licha ya habari hizo za kupangishiwa mjengo na kigogo serikalini mwenye cheo cha uwaziri kuenea kwenye mitandao ya kijamii wapambe wa mwanamitindo huyo wamekuwa wakimtetea kwa kuwashambulia wale wanaoona kuwa Mobeto hawezi kufanya mambo makubwa mpaka awezeshwe na mwanaume.

“Kuna watu wana matope kichwani, kila siku Mobeto kafanyiwa hili mara lile na mwanaume ina maana kazi zote anazofanya hawezi kumudu kuendesha maisha yake?

 

“Hamisa ni mwanamitindo ni balozi wa bidhaa mbalimbali shughuli zote hizi analipwa fedha tena ndefu tu, anashindwaje kupanga nyumba bora ya kuishi?” Mmoja wa mashabiki wa Mobeto alihoji kwenye mtandao wa Instagram.

 

Risasi Mchanganyiko lilipomtafuta kigogo huyo wa serikalini kwa njia ya simu ili kumsomea tuhuma hizi hakupokea simu badala yake alituma ujumbe wa “Sorry, I can’t talk right now” akimaanisha kuwa hawezi kuongea kwa wakati huo.

 

Kutokupatikana kwake ndiko kumefanya Risasi Mchanganyiko lishindwe kumtaja jina pamoja na cheo chake lakini atakapopatikana na kuzungumzia skendo hiyo mambo yote yataanikwa bila kufichwafichwa.

STORI: MEMORISE RICHARD, RISASI

Leave A Reply