KIGOGO POLISI ALIYENASWA NA KABINTI KITANDANI, UTATA WAIBUKA!

SIKU nane baada ya kigogo aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa (RTO) kabla ya kustaafu, Mashaka Mdachi kunaswa ‘live’ kwenye kitanda cha chumbani kwake akiwa na ‘kabinti’ kadogo, utata umeibuka.  

 

Mdachi alikutwa akiwa na binti huyo wa shule ya msingi anayesoma darasa la tano (jina lake na shule vinahifadhiwa) akiwa naye ndani ya chumba chake kwenye nyumba anayoimiliki iliyopo Mtaa wa Area Five Kata ya Kichangani mjini hapa na kuibua taharuki kubwa kutokana na wingi wa wananchi walioshuhudia tukio hilo.

Kwa mujibu wa wananchi wa eneo hilo, kinachoendelea juu ya sakata hilo kinashangaza kwani hadi sasa kigogo huyo hajafikishwa mahakamani pamoja na kwamba ni tukio lenye ushahidi wa kila aina hadi picha. Baadhi ya wananchi hao ambao wamekuwa wakifuatilia tukio hilo kwa karibu walipiga simu kwa mwandishi wetu kutaka majibu ya kwa nini jamaa huyo hafikishwi mahakamani?

 

“Hapa tayari tunaona kuna utata, haiwezekani iwe kimya hivi na kigogo mwenyewe tunamuona tu mtaani (aliachiwa kwa dhamana akakamatwa tena na sasa yupo mahabusu), ukimya huu unashangaza au ndiyo ishu imekwisha hivyo?

 

“Tunachohitaji kwako mwandishi ni kujua mbona kama kuna figisufigisu kwenye ishu hii?” Alihoji mmoja wa wananchi hao aliyeomba hifadhi ya jina. Kufuatia hali hiyo, juzi Jumapili, mwandishi wetu alifika kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro, Kitengo cha Dawati la Jinsia na kuwakuta maafande wawili ambapo walipoulizwa walikiri kigogo huyo kutofikishwa mahakamani.

“Sisi siyo wasemaji wa Jeshi la Polisi, lakini ni kweli huyo Mdachi hatujamfikisha mahakamani. “Tunaendelea na upelelezi, kama unavyojua kesi inayomkabili ni nzito hivyo upelelezi ukikamilika tutamfikisha mahakamani,” alisema mmoja wa maafande hao.

 

Walipoulizwa wanapeleleza nini kwa muda wote wa siku nane wakati ushahidi wa picha upo unaonesha live mstaafu huyo akiwa na mwanafunzi huyo kitandani, maafande hao walidai wanaendelea kukusanya ushahidi zaidi wa tukio hilo.

Baada ya kutoka kwenye ofisi hiyo, mwandishi wetu alifika kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Willibrod Mutafungwa na kuelezwa na wasaidizi wake kwamba kamanda huyo kwa siku hiyo ya Jumapili hakuwepo ofisini.

 

Mwandishi wetu aliyekuwa na shauku ya kusikia majibu ya Kamanda Mutafungwa kuhusiana na tukio hilo alimpigia simu ambapo pia simu yake haikuwa hewani hivyo juhudi za kumtafuta kuelezea tukio hilo zinaendelea.

STORI: DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO

Je Rais Magufuli ‘Atawatumbua’ Maafisa Hawa?


Loading...

Toa comment