The House of Favourite Newspapers

Kigogo Simba Atoa Tamko kwa Mashabiki na Wanachama Kufunga Mjadala wa Uchaguzi

0

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amewataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo, kufunga mjadala wa uchaguzi uliofanyika juzi na badala yake wawaunge mkono wale wote waliochaguliwa kwa maslahi ya klabu.

Ally alisema, wakati wa uchaguzi kila upande ulikuwa na timu yake, hivyo kwa sasa wanarejea kwenye kauli mbiu yao ya Simba Nguvu Moja na kuendelea na mapambano ya kuijenga klabu yao wanayoipenda.

Simba walifanya uchaguzi juzi Jumapili ambapo Murtaza Mangungu akafanikiwa kutetea kiti chake kwa upande wa Mwenyekiti, huku Asha Baraka naye akifanikiwa kurejea kwenye Bodi ya Wakurugenzi upande wa wajumbe.

“Jukumu letu ni kuwaunga mkono wote waliochaguliwa kwa maslahi ya Simba, tukiwadhoofisha tumeidhoofisha Simba, tukiwapa nguvu tumeipa nguvu Simba.

“Hatuna muda tena wa kuendelea na mjadala wa uchaguzi, sasa tunarejea kwenye jukumu letu la msingi kucheza mpira,” alisema Ally.

Katika uchaguzi huo, Mangungu alishinda nafasi ya mwenyekiti, huku Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi walioshinda ni Dr Seif Ramadhan Muba aliyepata kura 1636, Asha Baraka (1564), CPA Issa Masoud Iddi (1285), Rodney Chiduo (1267) na Seleman Harubu (1250).

STORI: ISSA LIPONDA, SPOTI XTRA

JEZI za YANGA ZAWEKA REKODI, SIMBA WATOA TAMKO ZITO | KROSI DONGO

Leave A Reply