Kigogo Usalama Anaswa kwa Dawa za Kulevya – Video
MAMLAKA ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini inamshikilia aliyekuwa Afisa Usalama wa Shirika la Posta nchini, George Mwamgabe, kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Akizungumza na wanahabari makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna, James Lukas, amesema afisa huyo na wenzake walikamatwa kwenye oparesheni maalum iliyofanyika kipindi cha mwezi huu wa Septemba.
Kamishna James amesema afisa huyo alikuwa akishirikiana na wasafirishaji wa madawa hayo ambapo akiwa katika mahojiano alitoroka mpaka alipokamatwa wiki iliyopita.
Katika mkutano huo kamisha huyo na viongozi wenzake walimuonyesha afisa huyo na wenzake waliokamatwa na madawa hayo sehemu mbalimbali Dar es Salaamna Mwanza.
Wengine waliokamatwa kwenye oparesheni hiyo ni pamoja na Hassan Azizi, Hassan Shaban, William Sebastian, Hamdan Mwakilonga na Felix Odemba.
Kamishna huyo aliyataja madawa hayo kuwa ni heroini zaidi ya kilo moja na mirungi kilo 214.
Wakati akisema hayo alitoa tahadhari kwa wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuwaambia kwamba serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli iko makini katika kuwadhibiti na yeyote atakayeendelea kufanya biashara hiyo ataishia pabaya.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL
Comments are closed.