The House of Favourite Newspapers

Kigwangalla Amjibu Makonda Sakata la Idris na Picha ya JPM

WAZIRI  wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, amemjibu Mkuu wa Mkoa wa dar s salaam, Paul Makonda ambaye mapema hii leo amemtaka muigizaji maarufu wa vichekesho nchini, Idris Sultan kufika katika kituo chochote cha polisi.
Hii imekuja baada ya msanii huyo kuhariri picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuweka sura yake, pia kuhariri picha yake na kuweka sura ya Rais Magufuli kisha kuichapisha kwenye mitandao ya kijamiii ikiwemo Instagram na Twitter.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kigwangalla amesema; “Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo.”

Comments are closed.