The House of Favourite Newspapers

Kigwangalla, Mkenda Wakutana Mwanza, Sasa Kazi Tu!

0

BAADA ya kumaliza tofauti zao ndani ya muda uliotolewa na Rais John Magufuli, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana na Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo jijini Mwanza.

Viongozi hao wamekutana jana Januari 8, 2020,  kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha tatu cha maonyesho ya utalii kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kigoma na Tabora  na jukwaa la uwekezaji katika sekta ya utalii kwa kanda hiyo.

Pamoja na majadiliano ya maandalizi hayo, pia walipata fursa ya kupata kikombe cha kahawa pamoja ambapo kwa sasa viongozi hao wamedhamiria kufanya kazi za kumsaidia Rais Magufuli.

 

BREAKING: MOTO MKUBWA WALIPUKA KWENYE MATANKI YA MAFUTA KIGAMBONI…

Leave A Reply