Kihenzile Aongoza Ujumbe Wa Tanzania Red Cross Nchini Uswiswi
David Kihenzile, Rais wa Redcross Tanzania leo Oktoba 29, 2024 ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa 34 wa siku tatu wa Kimataifa(International Conference)Jijini Geneva Nchini Uswisi, unaendelea ukiwa umehutubiwa na Viongozi wakuu ikiwemo Ms Bercedes Babe Rais wa Steering Committee- Chombo kinachounganisha IFRC&ICRC duniani, Kate Forbes Rais wa IFRC na Mirijana Spoljaric Rais wa ICRC.
Mkutano huu unakutanisha Viongozi wakuu wa National Societies zote duniani( Tanzania Redcross ikiwa mmoja wapo) pamoja na Wawakilishi wa Serikali zote duniani.
Pamoja nami katika ufunguzi nimeaungana na Balozi Hoyce Temu Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa kwenye Mashirika ya Kimataifa, Geneva, Japhet Shirima Mwekahazina wa Redcross Tz Ms Lucia Pande Katibu Mkuu wa Redcross Tanzania pamoja na maafisa mbalimbali kutoka Serikalini.