The House of Favourite Newspapers

Kihenzile Atembelea Kiwanda Cha Kutengeneza Ndege Morogoro

0

Tayari ndege tano zimekamilika katika kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza ndege, kinacho itwa Airpalane africa limited ambacho hutengeneza ndege aina ya Skyleader 600 kilichopo mkoani morogoro.

Hayo yame semwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi davidi kihenzile wakati alipo tembelea kiwanda hicho na kusema kuwa haya yote yanatokana na uongozi thabiti wa Mhe Rais Dr Samia Suluh Hassan ambaye ndio chanzo cha kuongezeka kwa wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.

Aidha amesema kuwa kiwanda hicho kinacho milimiwa na wawekezaji kutoka jamuhuri ya Czech kimeanza rasmi shughuli zake mwaka 2022 ambapo mwaka jana 2024 kilifanikiwa kupata vibali vyote vya uwendeshaji na hivyo hadi sasa ndege tano zimesha tengenezwa na zina uwezi wa kubeba abiria wawili kila mmoja.

Hata hivyo ,ndege hizo zina weza kutumika katika shughuli mbalimbali hapa nchinkama vile kufanya tafiti za kisayansi,ulinzi,kilimo na kwenye swala zima la utalii.

Ndege hizi pia zina uwezo wa kutumia mafuta takribani lita 120 na kuruka angani kwa zaidi ya masaa saba bila kutua, jambo linaloonyesha mageuzi makubwa katika sekta ya anga nchini Tanzania.

POLISI WAONESHA VIDEO ya MUUAJI wa WATU 14 NEW ORLEANS AKIWASHAMBULIA POLISI KABLA ya KUUAWA…

Leave A Reply