The House of Favourite Newspapers

Kiiza aahidiwa minoti akiiua Yanga SC

0


KIIZA-1

Mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza.

Mohammed Mdose,Dar es Salaam
BAADA ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu siku hadi siku, mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza raia wa Uganda, amepewa ahadi ya kumwagiwa minoti na mashabiki wa timu hiyo iwapo tu ataifunga Yanga kwenye mchezo wa Jumamosi hii, na akawaahidi atafanya wanachokitaka.

Mashabiki hao walitoa ahadi hiyo Jumapili iliyopita mara baada ya mchezo kati ya timu hiyo dhidi ya Kagera Sugar uliomaliza kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku Kiiza akitupia yote.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika, mashabiki hao ambao walionekana kupagawa na kiwango cha mchezaji huyo walishindwa kujizuia na kuanza kummwagia minoti.

Wakati wanamkabidhi fedha hizo, walimpa ahadi ya kuwa mzigo kamili atapewa Jumamosi kama ataifunga Yanga na hizo zilikuwa ni kifuta jasho tu.

Mashabiki hao walisikika wakisema: “Bado Yanga sasa, chukua hizi za kifuta jasho kajiandae vizuri uzidi kutupa raha, kuna nyingine zaidi ya hizi zipo zinakusubiri siku hiyo.”

Wakati anapokea fedha hizo, Kiiza ambaye alionekana mwenye furaha hakusita kuwajibu mashabiki hao: “Msijali kazi yangu ni kufunga na siku hiyo nitafunga.”

Leave A Reply