The House of Favourite Newspapers

Kiiza agoma Simba, kocha amtuliza

0

KIIZA-1KINARA wa mabao katika Ligi Kuu Bara, Hamis Kiiza, jana Ijumaa aligoma kuendelea na mazoezi ya asubuhi na wenzake baada ya kutoridhishwa na mwamuzi wakati akijifua na kikosi chake cha Simba Uwanja wa Amaan.

Ishu nzima ilikuwa hivi, katika mazoezi ya jana asubuhi, Kocha Dylan Kerr aliamua kupanga vikosi viwili ambavyo vilipambana huku mwamuzi akiwa Kocha wa Makipa, Idd Salim.

Sasa wakati mazoezi hayo yakiendelea, straika Pape Nd’aw alicheza faulo na mwamuzi kupeta ndipo Kiiza alipokasirika na kususia ‘mechi’ hiyo kwa kutaka kutoka uwanjani.

Kocha msaidizi, Selemani Matola kwa kushirikiana na wachezaji wenzake walimsihi aendelee na mazoezi, lakini Kiiza alikataa, ndipo Kerr ambaye alichezea upande mmoja, alipomfuata na kumsihi straika huyo kuendelea na mazoezi.

Kiiza alikubali kuendelea na mazoezi hayo na upande wake ukapata ushindi wa mabao 5-4. Simba iliondoka visiwani hapa jana mchana kwa ndege kwenda Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Yanga.

Leave A Reply