The House of Favourite Newspapers

Kiiza arudi Uganda

0

kiiza mbwembweMshambuliaji wa Simba Hamis Kiiza.

Wilbert Molandi,Dar es Salaam
KASI ya mabao anayoendelea kuionyesha kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara, imemshawishi Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ Mserbia, Milutin ‘Micho’ Sredojevic kumrejesha kikosini, Hamis Kiiza.

Mshambuliaji huyo, mara kwa mara amekuwa akitemwa na wakati mwingine kurejeshwa kwa kile kilichoelezwa uwezo wake wa ndani wa uwanja kupanda na kushuka.

Lakini kocha huyo, safari hii amemuita staa huyo anayeongoza kwenye ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao 18 akifuatiwa na Amissi Tambwe mwenye 17.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kiiza alisema juzi Jumapili alipokea barua aliyotumiwa kutoka Shirikisho la Soka Uganda (Fufa) likimuhitaji kuripoti kwenye kambi hiyo.

Kiiza alisema, amepanga kuondoka nchini kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho cha The Cranes mara baada ya mechi ya ligi kuu dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

“Ninashukuru kuitwa timu ya taifa kwa mara nyingine, ni jambo la heri kwangu kuitwa ni heshima kubwa katika maendeleo ya soka.

“Nimepokea barua kutoka shirikisho la soka la Uganda Jumapili iliyopita ikinitaka niripoti kwenye kambi ya timu ya taifa, hivyo nimepanga kuondoka baada ya mechi ya Coastal Union,”alisema Kiiza.

Leave A Reply