The House of Favourite Newspapers

Kiiza azungumzia usajili wa Kavumbagu Simba

0

kiiza

Mshambuliaji wa Simba, Mganda, Hamis Kiiza.

Wilbert Molandi,Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Simba, Mganda, Hamis Kiiza, amemkaribisha Mrundi wa Azam FC, Didier Kavumbagu, kujiunga na timu hiyo inayofundishwa na Muingereza, Dylan Kerr.

Hiyo ni siku chache tangu ziwepo tetesi za Mrundi huyo kuomba kujiunga na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu kwa mkopo.

Mrundi huyo, hivi sasa hana nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Azam tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kwa kile kinachodaiwa kuwa mshambuliaji huyo ameshindwa kumudu mfumo wa Kocha Mkuu Muingereza, Stewart Hall.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kiiza alisema kuwa, anatambua uwezo wa mshambuliaji huyo ndani ya uwanja, hivyo anaamini akitua kuichezea timu hiyo, ataiboresha safu yao ya ushambuliaji.

Kiiza alisema kikubwa anataka kuona safu yao ya ushambuliaji inaimarika kwa kuwepo na washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.

“Katika timu lazima wawepo washambuliaji zaidi ya watatu ambao ni tishio kwa wapinzani, lakini siyo kuwepo mmoja ambaye mabeki wa timu pinzani wenyewe wanamuangalia yeye tu katika kumkaba.

“Hivyo kama Kavumbagu anataka kuja Simba, mimi namkaribisha, ni mshambuliaji mzuri niliyecheza naye timu moja ya Yanga, ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, pia anajua kupambana,” alisema Kiiza.

Leave A Reply