The House of Favourite Newspapers

Kiiza bado hali ngumu bwana

0

KIIZA-1

Straika wa Simba, Mganda, Hamisi Kiiza.

Omary Mdose
STRAIKA wa Simba, Mganda, Hamisi Kiiza, leo Jumatano anaweza kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara wakati timu yake itakapopambana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kutokana na kutokuwa fiti asilimia mia.

Kiiza ambaye bado hajapona vizuri majeraha ya nyama za paja, tayari ameanza mazoezi tangu wiki iliyopita lakini kwa tahadhari kubwa.

Katika mazoezi ya juzi Jumatatu waliyoyafanya Simba kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kiiza alifanya mazoezi lakini mara kwa mara daktari wa timu hiyo, Yasin Gembe, alikuwa akimwambia awe makini ili asijitoneshe.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Muingereza, Dylan Kerr, aliliambia gazeti hili kuwa, hawezi kumlazimisha Kiiza kucheza mechi ya leo kwani anajua hatari ya kumchezesha mchezaji mwenye majeraha.

“Kiiza bado hajawa fiti kwa asilimia mia, hivyo siwezi kumlazimisha kucheza dhidi ya Coastal kwani najua hatari ya kufanya hivyo kwa mchezaji ambaye hajapona vizuri, ninao wachezaji wengi, hivyo nitawatumia kama mbadala wake,” alisema Kerr.

Leave A Reply