The House of Favourite Newspapers

Kiiza kimya kimya Mbeya City

0

STRAIKA wa Simba, Hamis Kiiza bado hajapona majeraha ya nyama za paja, lakini timu yake imepambana na leo anaweza akacheza dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, usibishe.

Kiiza ambaye jana Ijumaa alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake akitimiza miaka 25, juzi Alhamisi alianza mazoezi mepesi ambayo kitabibu alipaswa kufanya kwa wiki nzima ndipo apambane katika mechi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, mmoja wa viongozi wa Simba ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema: “Kama mambo yakienda vizuri, Kiiza atacheza dhidi ya Mbeya City ili kuongeza nguvu kikosini, usitake kujua tutafanya kitu gani.”

Alipoulizwa na gazeti hili juu ya mpango huo, Kiiza alitabasamu kisha akasema:  “Jamani, mimi bado nina majeraha ya nyama za paja na sitoweza kucheza kesho (leo), naumia moyoni kuikosa mechi hii, pengine ningefunga.”

Kiiza aliumia katika mazoezi ya Simba baada ya mechi dhidi ya Yanga na alitakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili. Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema: “Kuna uwezekano mdogo wa yeye kucheza.”

Leave A Reply